Waziri
wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Nape Nnauye jana March 20, 2017
alifanya ziara makao makuu ya Clouds Media Group baada kuwepo taarifa
za Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kwenda kwenye kituo hicho
akiwa na askari wenye silaha na kuwataka watangazaji wa Kipindi cha
SHILAWADU kurusha kipindi chake.
Waziri
Nape aliunda Tume ya uchunguzi ya watu watano wakiongozwa na Mkurugenzi
wa Habari Maelezo na kutoa saa 24 kwa tume hiyo kuzungumza na Makonda
na watu wake kisha leo March 21 iwasilishwe.
Baasa
ya kuona anapigiwa simu nyingi za kuhoji hatua iliyofikiwa hadi sasa
Waziri Nape ametoa majibu kupitia Account yake ya Twitter na kusema :"Kuna
simu nyingi juu ya ripoti. Nawaomba tutulie Kamati wanamalizia kazi
yao, ikikamilika tutataarifiwa muda na mahali nitakapokabidhiwa!
SHARE NA WENZAKO."
Comments
Post a Comment